Zaburi 122

1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani mwa Mwenyezi Mungu.”

2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako.

3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ulioshikamana pamoja.

4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Mwenyezi Mungu, kulisifu jina la Mwenyezi Mungu kulingana na maagizo waliopewa Israeli.

5 Huko viti vya hukumu hukaa, viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi.

6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wanaokupenda na wawe salama.

7 Amani na iwe ndani ya kuta zako, na usalama ndani ya ngome zako.”

8 Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu, nitasema, “Amani iwe ndani yako.”

9 Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.