Ndipo huyo mwanamke akaenda kwa watu wote akiwa na ushauri wake wa busara, nao wakakata kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumtupia Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wake wakatawanyika kutoka mjini, kila mmoja akirejea nyumbani mwake. Naye Yoabu akarudi kwa mfalme huko Yerusalemu.
Nakili HTML hii kwenye tovuti yako — matumizi huru, bila funguo, bila kufuatiliwa. Ongeza ?theme=light au ?theme=dark kwenye anwani ili ilingane na ukurasa wako.