Zaburi 129

1 Wamenitesa sana tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

2 wamenitesa sana tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

4 Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.

5 Wale wote wanaoichukia Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.

6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”