Zaburi 123
1 Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi.
2 Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mjakazi yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hadi atakapotuhurumia.
3 Uturehemu, Ee Mwenyezi Mungu, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi.
4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.